Facebook RSS RSS GUMZO LA JIJI | Pata Habari Moto moto
Headlines :

Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kila siku kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini..!!


BOMU LALIPUKA NA KUWAJERUHI WANAFUNZI 7 WA NABOTI SEKONDARI HUKO IRINGA...!!

Saturday, May 25, 2013 | 5:16 PM

 Baadhi ya Maeneo walimo jeruhiwa wanafunzi hao na Mmoja kupatwa na Mshtuko wa Mlipuko wa Mabaki ya Mabomu hayo kutokana na Tatizo lake la Moyo alilonalo na hivyo kupelekea wanafunzi Watano kulazwa Ilembula Hospitali.
 Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akiwajulia Hali wanafunzi hao katika Hospitali ya Lutherani ya Ilembula.
 Mwanafunzi Evance Joseph[16]kidato cha Kwanza ambaye alikuwa akifanya Majaribio ya Kuchoma Mabaki hayo ya Bomu huku Mengine akiyahifadhi kwenye Tranka lake la Nguo.
 Wanafunzi wakiwa wanaendelea kufanyiwa Vipimo vya Mionzi ya Jua kutambua ukubwa wa Tatizo  katika Hospitali ya Ilembula Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe.
 DC Njombe na Msafara Wake wakiwatazama Wanafunzi waliojeruhiwa na Mabaki ya Mabomu hayo.

 Mwanafunzi aliyejeruhiwa Katika maeneo Mbalimbali ya Mwili wake ikiwemo Miguuni.
 Hapa Mkuu wa Wilaya na Msafara wake ukiongozwa Na JWTZ Makambako.
 Msafara ukiwasili katika Shule ya Sekondari NABOTI Iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako.
 Wanafunzi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Njombe.
 Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari NABOTI Mara baada ya kutoka katika Hospitali ya Ilembula kuwajulia Hali wanafunzi Watano waliolazwa kwa Matibabu.
 Wanafunzi wa NABOTI Sekondari wakimsikiliza DC na Msafara wake.
 
Wanafunzi Wanne wa shule ya sekondari NABOTI iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako wamejeruhiwa na Mlipuko wa Mabaki ya Bomu huku mmoja akipata Mshtuko wa Moyo kutokana na Mlipuko huo Baada ya Wanafunzi Takribani saba wa Kidato cha Kwanza kwenda kuyaokota Mabaki hayo kwenye Mlima uliopo Jirani na maeneo ya Jeshi.


SOURCE: KALI ZA KITAA
Blogger Tricks

"MWANAMKE MCHAWI ADONDOKEA KANISANI AKIWA NA BIBLIA MKONONI, WAUMINI WAHAHA, YEYE MWENYEWE ANENA MAZITO "...!!

Wakati Mtwara kukilipuka kwa vurugu za gesi na kusababisha maafa, jijini Dar kumeibuka taharuki ya aina yake baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Anna kudaiwa kuwa ni mchawi na kudondokea kanisani.


Tukio hilo lililochukua saa kadhaa lilitokea katika Kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji linaloongozwa na Nabii Flora Peter lililopo Mbezi Beach Salasala, Dar hivi karibuni.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni waumini wa kanisa hilo inadai kuwa mwanamke huyo, mkazi wa Bunju, Dar alifika kanisani hapo saa 4:45 asubuhi huku akiwa amebeba Biblia na pochi lake akionekana kuwa sawa waumini wengine.

WAUMINI WABAKI VINYWA WAZI
Ilidaiwa kuwa muda mfupi baada ya maombi kuanza, katika hali isiyo ya kawaida, mwanamke huyo aliruka kupitia dirishani akapotea na kuacha waumini vinywa wazi.
Habari zilidai kuwa kuna baadhi ya watu walimuona kwenye paa ya nyumba ya watu waliojenga karibu na kanisa hilo, hali iliyozidi kusababisha mkusanyiko mkubwa wa watu wakiwemo askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) waliokuwa wakimshangaa.
Wakati taharuki hiyo ikiendelea, mwanahabari wetu alitonywa kuwepo kwa tukio hilo ambapo aliwasha ‘tukutuku’ yake na kuwahi eneo la tukio.


NI SIMULIZI NDEFU
Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa viongozi wa kanisa hilo aliyejitambulisha kwa jina la Octavian Mahembe alikuwa na haya ya kusema:
“Nakumbuka kulikuwa na waumini wengi kanisani, walikuja kwa ajili ya maombi, huyo mwanamke naye alikuja hapa kama waumini.
“Ilipofika saa 5:00: asubuhi watu wakawa wanasubiri maombi, baadaye nabii naye akawa amefika na kuanza kutoa maombi. Baada ya maombi kuanza, yule mwanamke alianza kuhangaika, akawa anahamahama, hatulii sehemu moja.


“Watu waliokuwa wanataka kuombewa waliambiwa wapite mbele.
“Yule mwanamke alikurupuka na kurukia ukuta wa futi sita na nusu, akadondoka nje.
“Nabii alisema afuatwe ili aombewe, alidai kwa kuwa si mtu mwema ni hatari na anaweza kuliangamiza kanisa na waumini kwa jumla kwani alikuwa na nguvu za giza.
“Alipochukuliwa akapelekwa kwa Nabii, akaombewa sala ya toba huku akikataa kwa kusema hana dhambi.
“Aliendelea kuombewa na baada ya maombi alitoka nje kupitia mlangoni. Akiwa nje alivua nguo na kubaki na ile ya ndani tu, akapanda juu ya paa la nyumba jirani na kanisa, akarukia nyumba nyingine juu kwa juu bila kushuka.
“Hakuishia hapo, akawa amerukia mti huku akionekana kama mtu wa ajabu kiasi kwamba hata watu wengine hawawezi kufanya yale aliyokuwa akiyafanya.
“Watu wengi walikusanyika wakiwemo polisi na wanajeshi. Baada ya kupotelea mitini, ghafla kilisikika kishindo kanisani baada kudondoka eneo hilo.
“Baadaye alipelekwa ofisi ya serikali ya mtaa kwa usalama wake kwani watu walitaka kuchukua sheria mikononi wakidai ni mchawi,” alimaliza kusimulia kiongozi huyo wa kanisa.




ATANGAZA ALIYOKUWA AKIFANYA
Hata hivyo, habari nyingine zilidai kwamba kabla ya mwanamke huyo kupelekwa serikali ya mtaa, wakati akiombewa alikuwa akitangaza mambo mengi aliyokuwa akiyafanya yasiyoeleweka kwa watu wasiojua mambo ya kilozi.
 
SERIKALI YA MTAA
Mwandishi wetu hakuishia hapo, alikwenda hadi ofisi za serikali za mtaa kutaka kujua kama mwanamke huyo alifikiswa hapo na sehemu alipo kwa sasa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Salasala, Monica Timba alikiri kutokea kwa tukio hilo akidai kuwa siku hiyo hakuwepo ofisini lakini alipigiwa simu na mkazi wa eneo lake kujulishwa juu ya tukio hilo.
“Niliambiwa kuna vurugu kubwa katika mtaa wangu na kwamba kulikuwa na mchawi amedondoka kanisani,” alisema mwenyekiti huyo.
Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa  baada ya kupewa taarifa hiyo alimpigia simu mtendaji wake, Ramadhan Juma ili mwanamke huyo aokolewe na walifanya hivyo.



HADI KITUO CHA POLISI
Alisema kuwa baadaye mwanamke huyo alipelekwa kituo kidogo cha polisi kilichopo eneo hilo cha Mtongani.
Risasi Jumamosi lilibisha hodi kituoni hapo na kuzungumza na askari aliyekuwa zamu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo ambaye alikiri kuripotiwa kwa tukio hilo kituoni hapo.
“Ni kweli huyo mwanamke alifikishwa hapa akidaiwa ni mchawi lakini baadaye tulimwachia kwa sababu sisi hatuamini mambo ya uchawi,” alisema.    

"MIMI NA WANAUME DAMU DAMU".....WEMA SEPETU

HABARI zinasema kwamba staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, ‘Beautiful Onyinye’ ameongeza idadi ya wanaume katika uhusiano wake na kuzidi kuwa katika chati ya magazeti ya Bongo, Risasi Jumamosi lina habari kamili

Wema ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Endless Fame, anadaiwa kuwa beneti na kijana aitwaye Robby lakini mwenyewe amesema kwamba hakuna anayeweza kumtenganisha na wanaume.
Habari zinasema kuwa, Wema na Robby wamekuwa wakipiga picha za kimahaba na mnyange huyo kuziingiza kwenye mtandoa wake na kumtambulisha kijana huyo kwa jina la ‘Honey’

Risasi Jumamosi lilifanya juu chini na kumsaka Wema ili kumtaka ajibu tuhuma za kuwa katika mahaba na kijana huyo.

Mei 22 mwaka huu, mwandishi wa gazeti hili alifika ofisini kwa mrembo huyo, Mwananyamala Komakoma jijini Dar es salaam na kumbana kwa maswali juu ya kuvuja kwa picha zake hizo akiwa na Robby na nyingine akiwa na wanaume wengine tofauti.


“Watu wamekuwa wakinizungumzia kila kukicha, tena maongezi yao yamekuwa yakianzia kwenye baadhi ya picha zangu, kila mtu ana namna ya kutengeneza ‘laifu’ yake na miye huwa sioni shida mwanaume asiye hawara yangu kunikisi au miye kumkisi,” alianza kujitetea.


“Ukifuatilia historia yangu mara nyingi utagundua marafiki zangu wengi ni wanaume kuliko wanawake na wengi wao wanakuja kwangu, tunakunywa na wanaondoka mida mibovu, kwa asiyenijua anaweza kuhisi ni mabwana zangu kumbe siyo, hata kwenye mitandao huwa sioni tabu kuweka picha za mtu akinikisi au nikimkisi,” aliendelea kusema.
 

“Siwezi kubadilika hii ni life style yangu. Siwezi kuacha kuwa karibu na marafiki wa kiume, hivyo ndivyo nilivyoumbwa watu wasinishangae, suala la kukutana na mtu na kupiga naye picha siyo ishu kwangu, ningekuwa mtu wa ajabu sana kama ningekuwa nawakisi midomoni au wao kunikisi mdomoni,” aliongeza.
Wema amesema kuwa watu wana hisia mbaya juu yake na Robby jambo ambalo siyo sahihi kwa kuwa, katika maisha yake anawapenda marafiki wa kiume zaidi ya wanawake.

RIPOTI MAALUMU KUHUSU KUACHIWA HURU KWA "RAMA MLA WATU' ...!!


Ramadhani Suleiman 'Rama mla kichwa' (kulia) na mama yake mzazi, Khadija (katikati) walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza.
------------
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemuachiwa huru Ramadhani Suleiman (Rama mla kichwa) aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya mauaji, baada ya kubaini hana akili timamu.

Jaji Rose Temba alitoa hukumu hiyo jana kutokana na ripoti ya Dk Mdeme Erasto iliyowasilishwa mahakamani hapo kuonesha kuwa, wakati mshitakiwa huyo anatenda kosa hilo hakuwa na akili timamu.


Ramadhani, ambaye alishitakiwa pamoja na mama yake Khadija Suleiman, alidaiwa kukutwa na kichwa cha mtoto Salome Yohana (3) katika eneo la Hospitali ya Taifa Muhimbili kikiwa katika mfuko wa plastiki maarufu kama rambo.


 Jaji Temba alisema mshitakiwa alitenda kosa la mauaji, lakini kwa kuzingatia ripoti ya uchunguzi wa akili, mahakama haiwezi kumtia hatiani hivyo aliamuru mshitakiwa huyo awe chini ya uangalizi wa madaktari wa Hospitali za magonjwa ya akili na watatakiwa kuripoti maendeleo ya afya yake kwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Aidha mahakama ilimwachia huru mama mzazi wa mshitakiwa huyo, Khadija, kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) hakuwa na haja ya kuendelea kumshitaki.

Awali Wakili wa utetezi, Yusuph Shehe alidai kuwa mahakama ilitoa amri ya mshitakiwa kwenda hospitali kuchunguzwa kama ana akili na ripoti ya daktari iliwasilishwa mahakamani hapo na kubainisha kuwa hakuwa na akili timamu, hivyo aliomba mahakama imfutie mashitaka.

Akiwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao, Wakili wa Serikali Cecilia Mkonongo alidai kuwa Aprili 25 mwaka 2008 saa 2:25 usiku, Salome (marehemu) alikuwa anacheza na Ramadhan pamoja na mtoto Paschal Lucas lakini baadaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha.


Alidai saa 2:30 usiku baba wa Salome, Yohana Mussa alikwenda kwa dada yake aitwaye Furaha ambapo Salome alikuwa akiishi, alipohoji mtoto wake yupo wapi ndipo wakaanza kumtafuta bila mafanikio, wakaamua kutoa taarifa kwa balozi.

Aliendelea kudai kuwa, asubuhi ya Aprili 26 mwaka 2008, wakiwa  njiani kwenda kituo cha polisi walipewa taarifa kuwa kuna kiwiliwili cha mtoto kimeonekana katika choo cha nyumba ya washitakiwa, walipokwenda walikuta mwili wa Salome ukiwa chini bila kichwa.

Mkonongo alidai wakiwa katika eneo la tukio, polisi walipata taarifa kuwa kuna mtu amekamatwa na kichwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, walikwenda wakiwa na askari na ndugu wengine na kukitambua kichwa hicho.

Ilidaiwa kuwa, Ramadhani alikamatwa na mlinzi wa Hospitali hiyo akiwa na kichwa hicho na kudai anakipeleka kwa shangazi yake anayefanya kazi ya usafi katika hospitali hiyo.

Aprili 29 mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na ripoti ya daktari ilionesha,  chanzo cha kifo chake hakikujulikana lakini, ilidai Salome alikatwa na kitu chenye ncha kali na alikuwa na michubuko mwilini.
 

Rama alipohojiwa na askari, alikiri kukutwa na kichwa hicho na kudai mama yake ndiye aliyemuua Salome kwa kutumia shoka na alikuwa anapeleka kichwa kwa shangazi yake.
 

Mama wa mshitakiwa huyo (Khadija)  alipohojiwa alikiri mwili wa marehemu kukutwa kwenye choo chake na ukiwa umefungwa na shati la Ramadhani.
 

Baada ya uamuzi huo kutolewa, ndugu wa marehemu waliangua kilio, na walipotoka Upendo Dunstan (mama wa marehemu) na shangazi yake Furaha Mussa walikuwa wakiangua kilio huku baba wa mtoto akilia huku ameshika kiuno nje ya mahakama hiyo. 


Washitakiwa walirudishwa rumande kwa ajili ya kukamilisha taratibu, baada ya kusota rumande kwa zaidi ya miaka mitano.

JWTZ YAKANUSHA TAARIFA ZA ASKARI WAKE KUJIHUSISHA NA UBAKAJI HUKO CONGO...!!


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ, limekanusha taarifa zilizotapakaa kwenye mitandao kuwa askari wa jeshi hilo waliokwenda huko kwa ajili ya kulinda amani,wameanza kujihusisha na makahaba.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Mtandao wa www.congodrcnews.com umedai wanajeshi wa Tanzania wameanza kujihusisha na ubakaji wanawake katika Mji wa Sake ulioko Goma.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa askari mmoja wa JWTZ alihitaji kujamiiana na mwanamke mmoja(Kahaba) kwa ujira wa Dola 50. Baada ya kumaliza shida zake ambazo ilielezwa alizifanya bila kinga yoyote,askari huyo alikataa kumlipa ujira wake,hali iliyoleta tafrani na mwanamke huyo kupiga kelele.

“JWTZ linapenda kuwaeleza wananchi kuwa taarifa hizo ni za uongo mtupu wenye nia ya kulipaka matope JWTZ na Tanzania kwa ujumla. “Picha iliyotolewa kwenye tovuti hiyo ya www.congodrcnews.com ni ya wanajeshi wa Tanzania walipokuwa katika Operesheni ya huko Comoro mwaka 2008.

Mtu anayeonekana kuwa chini ya Ulinzi alikuwa ni mshiriki wa Kanali Mohamed Bacar ambaye aliondolewa madarakani.

“Vilevile picha hiyo ilitolewa vile vile katika tovuti za www.apc.net.au/news/stories ya Machi 26, 2008 na ww.Seattletimes.com. na pia picha hiyo ipo pia kwenye tovuti ya Jamii Forum baada ya kufanya ‘link’ kutoka kwenye Mtando wa www.google.com.”

Taarifa hiyo ilisema kuwa JWTZ inapenda kueleza wananchi na dunia kwa ujumla kwamba wanaoneza taarifa hizo wana lengo la kukatisha tamaa juhudi zinazofanywa na nchi za Maziwa Makuu na SADC kuleta amani nchini DRC kwani JWTZ wako DRC kwa mujibu wa taratibu za kiutendaji za Umoja wa Mataifa.    

KIBAKA ALA KICHAPO CHA MBWA MWIZI NA KUNUSURIKA KIFO WAKATI AKITAPELI MTU HUKO KINONDONI...!!

KWA muda mrefu Gumzo la jiji limekuwa likipokea malalamiko kuhusu uwepo wa jamaa anayedaiwa ni tapeli maarufu Dar kisha kuingia mzigoni na kumnasa ‘laivu’ ambapo alihenyeshwa kwa kibano cha karne na raia waliokuwa na hasira.



Mtego huo ulifyatuka Jumanne ya Mei 21, mwaka huu ambapo kijana mmoja (jina halikupatikana) alinaswa na kupewa ‘henyahenya’ ya aina yake huku akinusurika kuchomwa moto.
Bila kujua kuna mtego, kijana huyo aliingia kwa mbwembwe katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar na kukaa katika moja ya viti kisha kuita mhudumu na kuchomoa noti ya shilingi ‘buku’ kumi, akaagiza misosi.
Akiwa amemeza tonge moja tu, aligeuka akatazama mlangoni, akamuona jamaa mmoja akimfuata kwa mwendo wa kasi na katika hali ya taharuki, ndipo akakurupuka akitaka kutoka nduki.


ILIKUWAJE?
Majira ya saa 9:00 alasiri, ghafla kijana huyo aliibua tafrani alipokurupuka mbio kutoka nje ya ukumbi huo.
Nyuma ya kijana huyo, jamaa aliyekuwa amedaiwa kutapeliwa na mtu huyo alianza kumkimbiza akipiga kelele za mwizi ndipo baadhi ya raia nao wakaanza kumfukuzia.


ATIWA MIKONONI
Raia hao walitimua mbio wakimfukuza kijana huyo na  walipofika maeneo ya Vijana, Kinondoni, kwa bahati mbaya alijikwaa na kuanguka ndipo akatiwa mikononi.
Yule jamaa ambaye alikuwa anamwitia mwizi, alikuja mbio na kuwaambia watu kuwa huyo ni tapeli ambaye alimtapeli shilingi laki tatu na nusu baada ya kumsomesha kuwa yeye ni mwajiri wa kampuni moja.
Aliyetapeliwa alidai kuwa katika utapeli huo, kijana huyo huwa anashirikiana na mzee mmoja ambaye huwa anavaa nguo nadhifu huku akiwa anatembea na  ‘briefcase’ mkononi.


‘ASACHIWA’
Jamaa huyo ‘aliposachiwa’ alikutwa na vitu kibao vya kitapeli yakiwemo makaratasi yaliyokatwa na kufungwa kwa noti bandia za shilingi elfu kumi zinazoonekana kama burungutu la fedha kumbe hakuna chochote ni ‘bosheni’.
Pia alikutwa na vitambulisho kibao vya watu vikiwemo vya kupigia kura, leseni na picha za ‘passport size’ za watu mbalimbali.
Katika makabrasha yake kulikutwa barua mbalimbali za serikali za mitaa za jijini Dar.
Alipoulizwa kuwa vitu hivyo vya watu na nyaraka za serikali ni vya nini au alivipataje, jamaa huyo alijitetea kuwa ana mtu anayeshirikiana naye katika michongo hiyo.


APEWA KIBANO CHA KARNE
Baadaye wananchi wenye hasira kali walichukua sheria mkononi na kumpa kibano huku akitakiwa kumpigia simu bosi wake aje eneo hilo.
Zoezi la kuja kwa bosi wake lilishindikana baada ya kupigiwa simu na kumkana hivyo baadhi ya watu walimvisha tairi la gari wakamwagia mafuta ya petrol, tayari kwa kumchoma moto.


Huku akiwa amehenyeshwa kwa kipigo na kulowa damu chapachapa, wakitaka kumchoma moto, madereva teksi wa eneo la Vijana, Kinondoni waliwakataza wasimchomee maeneo hayo kwani hawakutaka ushahidi hivyo wakamwachia akiwa nyang’anyang’a.

BREAKING NEWzz: KIONGOZI WA VURUGU ZA MTWARA AKAMATWA......!!

vujo mtwara

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                                                                    Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556                                                                                                           S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                                        DAR ES SALAAM.
24 MAY 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la Polisi Nchini linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi kwa tuhuma za kueneza ujumbe wa uchochezi na chuki kwa wananchi na viongozi wa serikali kwa njia ya simu ya mkononi akituma SMS kwa lengo la kuchochea fujo, vurugu na kutoa matusi kwa viongozi hao.

Mtu huyo amekuwa akifanikisha kazi hiyo kwa kutumia Chips (sim card) 13 za simu za mkononi ambazo amekamatwa nazo. Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji mtu huyo na ushahidi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zingine za wahahlifu kama hao kujitokeza na kutoa taarifa hizo polisi ili wahalifu hao waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki, wakiwemo watu wanaowashawishi wenzao kwa njia ya fedha, kuwashauri ama kuwasaidia kwa namna yeyote ile katika kufanikisha uhalifu huo na kusababisha uvunjifu wa amani hapa nchini.
Jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuvunja sheria za nchi.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

UPDATE:HATIMAYE RAMA MLA WATU AACHIWA HURU...!!

Friday, May 24, 2013 | 8:44 PM

Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeamua kumuachia huru Ramadhani Selemani Mussa ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na kichwa cha mtu. Rama, ambaye muda wote huo alikuwa rumande gereza la Segerea akisota kusubiri hukumu yake, alikamatwa hospitali ya Muhimbili mwaka 2008 ambapo pia alikiri kuwa alikuwa na tabia ya kula nyama za watu ambayo amefundishwa kichawi toka alipokuwa mdogo. Mahakama imemuachia huru kwasababu mtuhumiwa alitenda kosa hilo pasipo kuwa na akili timamu. Hata hivyo mahakama hiyo imetoa agizo la kuendelea kumuweka kijana huyo katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili, hospitali ya Isanga iliyopo Dodoma mpaka pale atakapona ndipo aruhusiwe kurudi mtaaani.habari kutoka karibu ndani 

HUYU NDIYE MWANAFUNZI WA CHUO ALIYEPIGA PICHA YA "UTUPU" ILI AFANANE NA RIHANNA...!!

 
Huyu ni mwanafunzi wa chuo(jina kapuni) aliyehamua kupiga picha ya utupu ili afanane na Rihanna Katika pozi...

Mwanafunzi Huyu ambaye yeye Binafsi anapenda kujifananisha na mwanamuziki asiyeishiwa na skendo Rihanna alifikia uhamuzi wa kujimulika na kamera na hatimaye kuficha....Ila ckuzote maovu ayajifichi.....

Picha hii ilisambaa mitandaoni hasa ya kijamii na hatimaye mdau wetu alitutonya na tukaipata...

Sio mbaya kama umefanana na mwanamuziki fulani ......ILA pia sio sahihi kuiga kila kitu ambacho mwanamuziki huyo anafanya...Kwa mtazamo tuu


TUNAJIFUNZA NINI...
Je ni sahii Kujimulika na katika picha za utupu ili tuuuu ujione umekamika na kufanana na mwanamuziki fulani........?

ANGALIZO.
TUMEFICHA SURA KWA KIUSALAMA WA MWANAFUNZI HUSIKA.....ILA TUJIFUNZE

TANGAZO MUHIMU KUTOKA KWA JESHI LA WANANCHI TANZANIA(JWTZ) KWA WANANCHI WOTE...!!

 " Mtanzania yeyote: kaa makini usiokote kitu chochote ambacho una mashaka nacho, kuna bomu zimerushwa toka nchi jirani Malawi zaidi ya 30 zenye uzito usiopungua tani 100. Hivyo basi uonapo kitu kipo kama chupa la chai chenye rangi ya fedha "usikiguse" piga namba 0756000042. SMS hii tuma kwa watu uwezavyo: Imetolewa na JWTZ/ LSL5CAMRM: Asante. "

"UHUSIANO WA KIMAPENZI BILA NGONO NI KUONGOPEANA".....TOPE OSOBA

Muigizaji Tope Osoba wa Nigeria, amekataa kuwa na mahusiano bila ya kukutana kimwili, na kufunguka kwamba anashangazwa na wasanii wengi wa Ghana na Nigeria wamekuwa wakiolewa na wanaume zao kuishi nje ya nchi kwa zaidi ya mwaka na hakuna kati yao aliyepata nafasi ya kumtembelea mwenzake.

Ngono ni kitu cha kuburudishana kati ya wawili wapendanao. Ngono ni nzuri. Imeumbwa ili wapenzi wa-enjoy na kubadilishana siri za mioyo yao.” Alifunguka actress huyo.
Alipoulizwa kuhusu mapenzi kabla ya ndoa, Tope alisema: “Mapenzi kabla ya ndoa ni poa tu, al muradi usalama kwanza. kwanza tusidanganyane, hauwezi kudumisha uhusiano bila ngono.”
Alifafanua kuwa maisha ya namna hiyo hayapo na kama yapo yana kitu nyuma ya pazi kwa kuwa hakuna mwaminifu bila ya sababu ya msingi
http://laivu.com/maraha/files/2013/05/tope-osoba_350.jpg

AIBU: MUME WA MTU ANASWA NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI GESTI...!!


INAUMA sana! Wakati wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili mabinti zao waweze kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo wapuuzi wanaokatisha jitihada hizo.

Mwanaume mmoja aitwaye Taliki Juma mkazi wa Temeke – Wailesi jijini Dar es Salaam ameingia  katika  dimbwi la AIBU baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili wakifanya mchezo mchafu.

 

Mbaya zaidi, bila haya wala soni, Taliki alimwingiza binti huyo (jina na shule anayosoma vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) katika chumba anachoishi na mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye alikuwa safarini.

Chanzo chetu cha habari kilipiga simu chumba cha habari na kueleza juu ya tabia ya Taliki ya kwenda na denti huyo chumbani kwake tena akiwa kwenye sare za shule.

Kikao cha dharura kiliitishwa haraka baada ya sosi wetu kutoa maelekezo juu ya habari hiyo ambapo kwa muda huo na foleni za jiji la Dar usafiri uliopendekezwa ukawa ni pikipiki.


Haraka timu ya waandishi  wetu ilielekea eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikwama.
 
Taarifa iliyopatikana kutoka kwa mtoa habari wetu ni kwamba, muda mfupi kabla timu haijaingia eneo la tukio, Taliki alifanikiwa kukwepa mtego baada ya kumuondoa denti huyo.


Wikiendi iliyopita Mei 18, mwaka huu chanzo chetu kilekile kilipiga tena simu kwa mwandishi yuleyule na kueleza kuwa jamaa kwa mara nyingine amemwingiza yule denti chumbani kwake.

Timu A iliondoka na kwenda moja kwa moja hadi eneo la tukio na kuliweka chini ya uangalizi huku timu B ikielekea katika Kituo cha Polisi cha Wailesi na kuomba ushirikiano wao.

Timu ya maaskari wa kituo hicho wakiwa tayari kwa lolote, waliungana na waandishi wetu kwenda eneo la tukio.

Waandishi wetu, maaskari na wazee wachache wa mtaani hapo walivamia katika chumba hicho na kufanikiwa kumnasa laivu Taliki akiwa na denti huyo kama walivyozaliwa akimfanyisha mambo ya kikubwa muda ambao alitakiwa kuwa darasani.


Binti huyo ambaye alionekana kushtuka sana baada ya kukutwa chumbani hapo, alieleza kuwa amekuwa katika uhusiano na Taliki kwa muda mrefu baada ya kumrubuni kwa fedha na zawadi mbalimbali.

“Ni kweli huyu hapa ni mpenzi wangu, huwa ananipa pesa. Nyumbani kwetu ni Mwananyamala na nimetoka nyumbani nikienda tuisheni lakini Taliki aliniambia nije kwake.
 

“Naombeni mnisamehe jamani. Mama akijua atanipiga sana. Nisameheni tafadhali na ninaahidi mbele yenu kuwa nitaachana kabisa na huyu mbaba (Taliki),” alisema denti huyo.
 

Denti huyo alitoa namba ya simu ya mama yake mzazi ambapo alipigiwa na kufika eneo la tukio na kujionea jinsi mtoto wake anavyoharibiwa wakati yeye akiwa kwenye juhudi za kumtengenezea maisha. 

Mama wa binti huyo, hakuamini alichokiona na alijikuta akimwaga machozi muda wote, watu wazima wakapata kazi ya kumtuliza.


UPUUZI WA TALIKI
“Ni kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye muda mrefu ila naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu alinipitia (Mh! Huyu shetani anasingiziwa mengi sana).
 
“Ndugu zangu wakijua hili jambo watanitenga, naombeni muwe na roho ya huruma (utadhani na yeye ana huruma), maisha yangu yataharibika (sijui alikuwa anamtengenezea yule binti  wa watu maisha?).”
 
Utetezi wake haukusaidia na badala yake alifikishwa katika Kituo cha Polisi Wailesi na kufunguliwa mashitaka katika Jalada namba WS/RB/585/2013 – KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.

AIBU: MCHUNGAJI ATEMBEZWA UCHI HADI KANISANI KWAKE BAADA YA MKEWE KUMFUMANIA NA MWANAKWAYA LIVE..!!

Mtumishi mmoja wa Mungu amejikuta akipata aibu ya mwaka si tu mbele za Mungu bali hata kwa mkewe pamoja na mashuhuda wengine baada ya mkewe kumfumania ‘live’ kitandani akifanya mapenzi na mwana kwaya wa kanisa lake huko Kisumu nchini Kenya.
 
Habari zilizoripotiwa na mtandao wa Kenyan-Post zinasema msichana huyo mweye miaka 23 amekuwa na mahusiano ya muda mrefu na pasta huyo kabla hawajabambwa.
 
Kisa hiki ni kama movie ambazo tumezoea kuziona zenye story line ambayo unaweza kutabiri mwisho wake.


 Kwa mujibu wa mtandao huo, ile ‘siku ya 40’ mke wa pasta huyo alikuwa anatarajia kusafiri kwenda nyumbani kwao kusalimia wazazi wake hivyo mumewe alimsindikiza mpaka kituo cha basi, lakini alionekana kuwa mtu mwenye haraka na kumwambia mkewe kuwa siku hiyo ana mkutano muhimu hivyo anapaswa kuwahi. Baada ya kumfikisha kituoni aligeuza gari kwa haraka na kuondoka.


Huku nyuma mke wa pasta kwa bahati mbaya (upande wa pasta) na bahati nzuri (upande wake) aligundua kuwa amesahau zawadi aliyokuwa amemnunulia mama yake mzazi ambaye ndio anaenda kumsalimia hivyo ikabidi airudie nyumbani kisha asafiri na basi litakalokuwa linafuata.
 
Alipofika nyumbani anapoishi na mumewe alishangaa kukuta mlango haujafungwa kwa nje na huku anakumbuka walipoondoka waliufunga hivyo akahisi huenda wamevamiwa mchana kweupe, alipojaribu kuusukuma ulikuwa umefungwa kwa ndani ndipo alipoomba msaada wa majirani wakavunja kitasa na kuingia ndani.
 
Mama huyo alipigwa na butwaa kwa kile alichokikuta ndani baada ya kumkuta msichana anayemfahamu kuwa kiongozi wa kwaya ya kanisani la mumewe wakiwa uchi wa mnyama katika kitanda chake na mumewe.

Maamuzi aliyochukua ni kuwavamia kitandani na kuzitupa nje kupitia dirishani nguo zao wote lakini kwa bahati mbaya msichana aliyemfumania alifanikiwa kukimbia na kumuacha pasta mwenyewe. 
 
Huwa wanasema hasira ni hasara na maamuzi ya hasira hugeuka majuto baadae, baada ya mmbaya wake kukimbia aliamua kumvuta mumewe (pasta) akisaidiwa na watu wengine  akiwa uchi wa mnyama na kumtembeza mbele ya umati wa watu mpaka katika kanisa analotoa huduma pasta huyo kwa lengo la kufichua mabaya yake.
 
Bahati nzuri alijitokeza mwanaume mmoja aliempatia shati lake ili ajisitiri.

WAASI WA M23 WATISHIA KUTUVAMIA MUDA WOWOTE....SERIKALI YA MKOA WA KAGERA YATOA TAHADHARI KWA WANANCHI

Serikali ya Mkoa wa Kagera imewatahadharisha wananchi wake kuepukana na wageni wasiowafahamu kwenye maeneo yao kutokana na tishio la kikosi chaM 23 cha nchini Congo DRC kinachotishia kuivamia Tanzania...
Kumekuwa na mapigano  makali  kati  ya waasi wa M23  na  vikosi vya serikali  nchini  Congo ambako jeshi letu lipo huko...
Waasi  hao  wametishia  kuivamia  Tanzania  muda  wowote  ili  kulipiza  kisasi.Miongoni mwa mipaka ambayo iko wazi  ni Kagera, na hii ndo sababu iliyopelekea  serikali ya Mkoa huo kutoa tahadhari kwa wananchi wake na watanzania kwa ujumla....

JACKLINE WOLPER NA BABY MADAHA WASHIKANA MASHATI WAKIGOMBANIANA NYUMBA YA KUPANGA


Sakata la wawili hao lilifika polisi na kubainika kuwa Madaha alilipa kodi kwa tapeli wakati Wolper alitoa fedha zake kwa mwenye nyumba hivyo kumfanya awe na haki ya kuhamia.
 

Akizungumza na mwandishi wetu, juzi jijini Dar es Salaam, Madaha alisema pamoja na kubainika kuwa alitapeliwa, mtu pekee ambaye angeweza kumsaidia kupata fedha zake (shilingi milioni tatu) ni Wolper lakini anamchenga.

“Ni kweli nimetapeliwa lakini Wolper kama msanii mwenzangu alikuwa na uwezo wa kunisaidia maana yeye anaishi pale lakini nimemwambia, ananipiga chenga. Sitaongea naye milele, hana utu kabisa. Milioni tatu ndugu yangu si pesa ndogo.”


KAULI  YA  WOLPER

Wolper alipotafutwa na kusomewa malalamiko ya Madaha alisema: “Naweza kusema Madaha hana akili, ni mpuuzi kwa sababu angekuja kwa busara nyumbani kwangu tungezungumza na baba mwenye nyumba tukajua namna ya kumsaidia.

“Lakini yeye kabla hajaomba ushirikiano kwangu, tayari naanza kusumbuliwa na magazeti kuwa eti nimemtapeli. 

Halafu hajawahi kunipigia simu bali alikuwa anawatuma watu wake kwangu. Kwa nini asingekuja mwenyewe?
 

“Ina maana yeye ni staa sana au? Huyu hana lolote anataka kupanda kwa kutumia jina langu,” alisema Wolper.

KIINGEREZA CHA UGOKO CHAMUUMBUA TENA DIAMOND INSTAGRAM....SOMA HAPA ALICHOANDIKA..!!

KWANZA  NAANZA  KWA  KUMPONGEZA  SANA  DIAMOND maana  akiwa hajamaliza hata wiki mbili tangu atoke kwenye tour iliyofanikiwa ya Burundi na Congo, Diamond leo amesaini mkataba wa show nyingine kubwa ya kimataifa.

Kupitia Instagram, Diamond ameshare picha inayomuonesha akisaini mkataba wa show huku pembeni akiwepo mtu mwenye asili ya Asia ambaye huenda ndio promoter. 

Kilichowafanya  mashabiki wake  huko instagram  wavunjike  mbavu  ni Kingereza  alichotumia.....
"After I DONE did the Uk,Congo,Burundi…guess where next I’ll be headed.”...

Haijalishi  umekosea au upo  sahihi, ujumbe  umefika  kaka!!.  Waache  wacheke, wataacha  tu.

 Hata  hivyo, si vibaya pia  kutumia  lugha  yetu ya kiswahili  maana  ujumbe  hufika  vizuri  zaidi....Kingereza lugha ya  watu...ni ngumu..!!! 

HATIMAYE DR. SLAA AKUBALIWA KUOANA NA MPENZI WAKE...





HATIMAYE Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na aliyekuwa mume wa Josephine Mushumbusi( KWA  SASA  NI  MCHUMBA WA DR. SLAA) , Maimbo baada ya kuiona rufaa hiyo haina msingi wowote kisheria.

Hukumu hiyo ya rufaa ya  madai ya ndoa Na.32/2012 ilitolewa leo na Hakimu Aniseth Wambura ambapo alisema mahakama yake imefikia uamuzi huo wa kuitupa rufaa hiyo kwasababu haina mantiki ya kisheria.

Hakimu Wambura alisema mahakama yake imekubalina na hukumu iliyotolewa Aprili 2012 na Mahakama ya Mwanzo Sinza katika kesi ya madai talaka iliyokuwa imefunguliwa na Mushumbusi anayetetewa na wakili wa kujitegemea Philemon Mutakyamilwa  dhidi ya Maimbo ambapo mahakama hiyo ya chini ilitangaza kuwa hakukuwa na ndoa baina ya watu hao kwasababu Maimbo alikuwa ni mzinzi, simwaminifu katika ndoa yake na alikuwa akimtesa mkewe.

“Baada ya mahakama yangu kusikiliza hoja za mwomba rufaa na mjibu rufaa ,mahakama hii imefikia uamuzi wa kukubali hoja za Mushumbisi kuwa kwa tabia ile ya mbaya ya uzinzi na ukosefu wa uaminifu katika ndoa yake hapakuwepo na ndoa baina yao hivyo mahakama yake inatangaza kuwa hukumu ya mahakama ya Mwanzo Sinza ambayo iliivunja ndoa hiyo ilikuwa hukumu sahihi “alisema hakimu Wambura.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili Mutakyamilwa alisema amefurahishwa na hukumu hiyo kwani mahakama imetenda haki  kwasababu kesi hiyo ya madai ya talaka ilikuwa na msukumo wa siasa chafu zilizokuwa na lengo chafu la kumchafulia jina mteja wake(Mshumbusi) ambaye kwa sasa ni mzazi mwenzie Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad Slaa.
KWA  HIYO, KWA  SASA  DR. SLAA   NA  MPENZI  WAKE  W ANAWEZA  KUOANA..!!!

"NINA MIAKA 26 LAKINI NIMESHINDWA KUACHA PUNYETO, NIFANYEJE?"... NAOMBENI USHAURI

Thursday, May 23, 2013 | 11:58 PM

Mimi ni kijana wa miaka 26 ninaandika hivi kwa sababu nimeamua kuomba mawazo kwa wa wanajamii, kwa ukweli na uwazi mimi ni mtu ambaye nimekuwa na tabia ya kupiga punyeto kwa muda mrefu hili tatizo lilianza kipindi fulani nipokuwa mkoa fulani hapa Tanzania, Nlikuwa na rafiki yangu mmoja na mpaka sasa bado ni rafiki yangu ni mtu mzima na ameoa pia ana watoto yeye ni mfanya biashara ya kununua na kuuuza madini. Alipokuwa akitoka porini kama amechelewa anapita geto kwangu tunalaa sasa tukaanzisha mchezo wa kushikana sehemu zetu za siri mpaka tunamaliza kitu tunachotaka japo hatuingiliani. Tuliendelea na mchezo huo kwa muda mrefu kwa sababu imekuwa mazoea.

 
Sasa tatizo langu liko hivi mimi kwa sasa niko nje kidogo na nchi yangu na yeye yuko na kazi zake za porini na akienda huchukua muda mrefu kurudi na mimi kulingana na mazoea inaniathiri kwa sababu kila ninapokumbuka ule mchezo namaliza nikiwa mwenyewe yaani yeye amekuwa kwenye kumbukumbu ya akilii yangu kwa sababu kuna siku tulifanya ule mchezo mpaka nikaona nimefika kileleni tofauti na wanawake niofanya nao mapenzi hakuna aliyetomasa mpaka nifikie hivyo. Na hii imenipelekea kila mwanaume ninayemwona kama ana umbo sawa na rafiki yangu natamani kufanya nae ule mchezo kitu ambacho kinakuwa ni ngumu. Na kila siku najaribu kujizuia kufanya huu mchezo ninashindwa sijui nitumie njia gani ili kuepukana na hili tatizo hili kubwa linalonisumbua.

LIKE UKURASA WETU HAPA..!!

HABARI MPYA

 
Support : Talkbongo | Gumzo Admin | Kwa Habari Moto moto!
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. GUMZO LA JIJI - Haki zote zimehifadhiwa
Original Design by GUMZO TEAM
Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter
UA-35914726-1